Thursday, 29 January 2015

MAN UTD, CHELSEA NA MAN CITY WASAFISHIA NJIA KWA POGBA.


Mino Riola ambaye ni wakala wa kiungo wa Juventus na timu ya taifa ya Ufaransa, Paul Pogba, amesema mchezaji huyo atakuwa sokoni majiraya joto na yoyote mwenye kitita cha kutosha anaweza kupata saini ya nyota huyo.
Paul Pogba
Kiungo huyo ambaye alijiunga na Juventus akitokea Manchester United mwaka 2012, amegeuka kuwa lulu nakuwindwa na vilabu mbalimbali vikubwa barani Ulaya ikiwemo klabu yake ya zamani Manchester United.
Pamoja na baadhi ya vilabu kuhitaji huduma ya kiungo huyo mwezi Januari, Riola amezima ndoto hizo kwa kusema kuwa mteja wake ataondoka majira ya joto.
Licha ya kusafisha njia kwa timu zinazomuwania Pogba, Riola ametandaza 'vipande vya chupa' kwa kusema kuwa timu inayomhitaji ni lazima iweke kitita cha kutosha.
"Nataka klabu itakayomnunua imuamini na iwe tayari kulipa kwa ajili yake. Kwa anayemuhitaji inaweza kumuwia hata zaidi ya yuro milioni 100," alisema Riola.
Ikumbukwe kuwa Pogba(21) ana mkataba na vibibi vizee hivyovya Turin mpaka 2019 na wakala wake huyo amsesema kuwa nyota huyo ana thamani na hadhi sawa na nyota wengine wakubwa duniani kama vile Messi, Cristiano Ronaldo, Zlatan Ibrahimovic na wengine.

Kauli hiyo itawafanya Louis Van Gaal, Jose Mourinho, Laurent Blanc, Manuel Pelegrini na wengine kuvunja benki mwishoni mwa msimu kushinda vita ya kupata saini ya nyota huyo.


YANGA INAVYOJINOA KUIVAA VIPERS KOMBE LA SHIRIKISHO


Na Ramadhani Ngoda. 
Uongozi wa Yanga SC umesema kikosi chake kitaweka kambi maalum kwa michuano ya kimataifa kisiwani Pemba na kitacheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya Vipers ya Ligi Kuu ya Uganda kabla ya kumenyana dhidi ya BDF XI katika hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwezi ujao.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Jerry Muro amesema jijini hapa leo kuwa kikosi chao kitaweka kambini kisiwani Pemba kujiandaa kwa mechi za mbili za hatua ya awali ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya BDF XI.
Amesema wametuma maombi kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mechi yao ya Februari 8 dhidi ya Mtribwa Sugar ipigwe kalenda ili wapate muda wa kutosha wa kukaa visiwani Zanzibar kujiandaa kwa michuano ya kimataifa. 

Yanga SC itacheza mechi yake ya kwanza dhidi ya timu hiyo ya Jeshi la Ulinzi la Botswana Febuari 14 kwenye Uwanja wa Taifa jijini na kurudiana mjini Gaborone wiki mbili baadaye.
Muro amesema wanatarajia kucheza mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Vipers (zamani Bunamwaya) ya Ligi Kuu ya Uganda kabla ya kuivaa BDF XI. 

Amesema mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa Uganda na kama timu hiyo ikija Tanzania, mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Amaan, Unguja visiwani Zanzibar ambako kambi yao itawekwa.


Awali Yanga SC iliripotiwa kuwa inataraji kuweka kambi maalum Afrika Kusini, Namibia na Zambia kabla ya kuwavaa maafande hao.

TFF YASIKITISHWA NA ZENGWE LA KESI YA ZFA

Rais wa TFF, Jamal Malinzi (mbele mwenye suti)  akiwasalimia wachezaji wa JKU walipochuana na Yanga kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi mwanzo mwa mwezi huu

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kuwepo tena kortini kwa kesi dhidi ya uongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA), jambo ambalo linaweza kuathiri ushiriki wa timu za Zanzibar kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, na Kombe la Shirikisho.

Mwishoni mwa mwaka jana, TFF ilihadharisha juu ya masuala ya mpira wa miguu kupelekwa mahakamani, kwani kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kitendo hicho ni kinyume cha taratibu za uendeshaji mpira wa miguu ambazo zinakataza masuala ya mchezo huo kupelekwa katika mahakama za kawaida.

Kutokana na hali hiyo, TFF iliiandikia barua ZFA kutaka mgogoro huo uondolewe kortini na yenyewe kuridhia kuwa tayari kupeleka ujumbe Zanzibar ili ukutane na pande zinazohusika.

Pia TFF ilisema timu za Tanzania Bara zisingeruhusiwa kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi 2015 iwapo kesi hiyo ingeendelea kuwepo kortini na kutaka iondolewe bila masharti yoyote.

ZFA iliithibitishia TFF kuwa kesi hiyo imeondolewa kortini bila masharti, hivyo timu za Tanzania Bara kuruhusiwa kushiriki katika michuano ya Kombe la Mapinduzi. Ni muhimu suala hilo likashughulikiwa haraka ili kutohatarisha ushiriki wa timu za KMKM na Polisi kwenye michuano hiyo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

'SUB' ZILIKUWA KISU CHA KUICHINJIA SIMBA- MWAMBUSI


Na Ramadhani Ngoda

Kocha Mkuu wa Mbeya City FC, Juma Mwambusi amesema mabadiliko katika kikosi chake aliyoyafanya kipindi cha mechi yao iliyopita dhidi ya Simba SC, ndiyo 'uchawi' ulioacha kilio Msimbazi.

Simba SC iliyokwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0, ilipoteza mechi yake ya pili msimu huu ilipopigwa 2-1 dhidi ya kikosi cha City Uwanja wa Taifa jijini hapa jana katika mechi yao ya kiporo cha raundi ya 10 yua Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Mechi hiyo ilipaswa kuchezwa Januari 11 Uwanja wa Taifa lakini ikapigwa kalenda na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na ushiriki wa Simba SC katika michuano ya Kombe la Mapinduzi 2015 visiwani Zanzibar ilikotwaa ubingwa.

Mara tu baada ya mechi hiyo, Mwambusi alisema mabadiliko aliyoyafanya kwa kuwatoa Themi Felix, Cosmas Lewis na Deus Kaseke kipindi cha pili yalikipa nguvu kikosi chake na kiizidi Simba SC kwa kila kitu.

Alisema kutoka kwa winga mkongwe anayeichezea kwa mara ya kwanza timu hiyo ya Jiji la Mbeya Ligi Kuu msimu huu, Felix dakika ya 69 ya mchezo kuliamsha mashambulizi mengi langoni mwa wanamsimbazi, hali iliyokifanya kikosi cha Mserbia Goran Kopunovic kipotezane uwanjani.

"Kuna tatizo la marefa, wakati mwingine wanafanya maamuzi kwa kushinikizwa na wachezaji, ninafikiri kipa wa Simba (Manyika Peter) alitakiwa kutolewa kwa kadi nyekundu.

Juma Mwambusi

"Mabadiliko tuliyofanya kipindi cha pili kwa kuwaingiza Hamidu (Mohamed), Idrisa Rashid na (Peter) Mapunda yalikipa nguvu zaidi kikosi chetu ndiyo maana kikawa kinafanya mashambulizi mengi na ya hatari na hatimaye kupata magoli," alisema Mwambusi.

Kocha Bora wa VPL msimu uliopita, Mwambusi alisema anaamini kikosi chake kitaendelea kufanya vizuri kwa vile kimerejesha makali yake ya msimu uliopita baada ya kufanya vibaya katika mechi za mwanzoni mwa msimu kikipoteza mechi nne mfululizo dhidi ya Azam FC, Mtibwa Sugar, Mgambo Shooting na Kagera Sugar.
   
Kipigo cha jana, kiliwaacha wachezaji wa Simba SC wakiangulia vilio mithili ya watoto huku kocha wao akiweka wazi kwamba timu hiyo ya Msimbazi haina nafasi ya kutwaa ubingwa msimu huu.

Simba SC itakuwa na kibarua kingine kigumu itakaposhuka tena Uwanja wa Tafa Jumamosi kumenyana dhidi ya JKT Ruvu Stars ya Pwani iliyoko nafasi ya tatu katika msimamo wa VPL ikiwa na pointi 18 sawa na Yanga SC iliyoko nafasi ya pili kwa faida ya tofauti nzuri ya mabao ya kufunga na kufungwa.

JKT Ruvu Stars inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga, mzawa Felix Minziro iliifunga Simba mabao 3-2 katika mechi yao ya mwisho msimu uliopita Uwanja wa Taifa. 

Kikosi cha Minziro msimu huu kinaoonekana kuwa moto wa kuotea mbali kwani ndiyo timu ya kwanza kuwafunga mabingwa waetezi Azam FC waliotwaa ubingwa wa VPL msimu uliopita bila kupoteza hata mechi moja.

Azam FC ilifungwa bao 1-0 dhidi ya JKT Ruvu Stars Uwanja wa Azam FC jijini hapa Oktoba 25 mwaka jana ikiwa ni kipigo cha kwanza kwa wanalambalamba baada ya kucheza mechi 38 za Ligi Kuu bila kupoteza hata moja.


Bao la kikosi cha Minziro lilifungwa na mshambuliaji hata kwa sasa VPL, Samwel Kamuntu ambaye amefunga mabao manne katika mechi nne mfululizo zilizopita. Kamuntu ana mabao sita kwa sasa msimu huu akizidiwa bao moja na kinara Didier Kavumbagu wa Azam FC.

Monday, 26 January 2015

YOUNGS PERFECT TO SAVE TENNIS IN TANZANIA

By Haruna Ramadhani
Kijitonyama Tennis Club head coach Mussa Haruna has insisted that only young generation can be used to save tennis in this country because they are more flexible and available than other ages.
The coach to stress that has asked parents to allow and support their children who seem to be interested in the sport.
“A parent who doesn’t support his/her child in the sport he/she is interested is a poison to child’s development,” Coach Mussa said.
Kijitonyama Tennis Club which uses the grounds owned by University of Dar-es-salaam to train they have been faced by a couple of challenges including trainees’ inconsistency.
“We started with almost 200 children but they never been consistent, we now have 20 or 25. At first the sport was lacking teachers, but now many teachers no trainees. You can how crazy is it,” emphasized Mr. Mussa.
Nevertheless the club have reached some successes including contributing players to the camped team for African Junior Championship (AJC) which expected to start next week at Gymkhana. The winner teams will be qualifying for African competitions.
“We have contributed at least 5 players, 3 girls and 2 boys who are now in the camp for AJC,”
In the other hand the trainees have never hesitated to be grateful to their coaches for their time and skills they give. 
“We appreciate them (coaches), they are very important to ourselves and our talents. They surely need us to be perfect in this sport. We love them a lot,” said Joyce John(13) who has joined the club just a month ago.
Joyce kept on adding that in the coming days Tanzania will have the likes of Mariah Sharapova and Victoria Wawrinka if the effort will be well put in tennis.

“I’m sure we have many Sharapovas and Wawrinkas of the coming days but not by relaxing and ignoring,” added Joyce
Meanwhile the assistant Coach Mr. Francis Knoute has gone direct to the reason as why many children fail to attend the club as failing to afford the training fee demanded by the grounds’ owners.
“From 200 to 25 trainees is very big step behind but you can’t stop it because some of them couldn’t afford to pay the fee. 50,000/= Tsh per year not many families can afford. It’s a challenge I can say,” Said Mr. Kanoute.
May be if we could have more free grounds hence the can train for free but for this we’ll still be having a low number of tennis trainee in our club,” he added.

PST NEEDS SUPPORT TO DEVELOP BOXING



By Ramadhani Ngoda.

Pugilistic Syndicate of Tanzania (PST) said that they alone can’t take boxing to higher stages and make it alive without support from stakeholders despite much effort they always put in it.

As one of the major supporters of boxing in the country, PST has been making steps including preparing various matches so as to provide entertainment to the supporters as well as boosting the boxers.

“Yes, we make a lot of effort to promote boxing in Tanzania as you can see but ourselves we can’t make it. There must be support from other stakeholders like sponsors if we really love boxing,” said PST general secretary, Antony Ruta.

When asked why still some boxers live in poor lives despite being successful in the game Ruta said that may is due to lack of plans in life by the boxers themselves. The secretary added that one will succeed in boxing if he really takes it seriously and not for prestige as some others do.

“If you are serious in boxing and have plans in your life you can’t live embarrassing life” added Ruta.
Francis Cheka akiwa ulingoni dhidi ya Thomas Mashali.


One of the famous Tanzanian boxing legends, Francis Cheka who won different tittles domestically and international has said that despite being a legend in the sport and winning a lot, still his life as good as of high profile boxer.

“I have won a lot but my life still like of the one who won nothing because you fight by expecting gate money. Not only that, you fight today and wait for four to six months to have another fight, how could you benefit then? You can’t,” said Cheka with lots of feelings.

Talking of his coming fight Cheka said that he does know neither amount to be paid nor the name of his opponent.

“I’m told I’ll have a fight against a British but I don’t know his name yet. I also know nothing about the amount of money I’ll earn,” he explained.

Kalama Nyilawila who also sets for his fight against Mada Maugo in March has said that sometimes one can think to quit boxing and keep doing other things to run life due to less profit of it. The issue being promoters to depend on the gate revenue to pay the boxers which sometimes fail

“Sometimes if feel like to quit. We can’t live depending on boxing, for what? Is that money from the gate revenue? No,” Said Nyilawila.

Speaking of defeats that Tanzanian boxers get when fighting outside the country Nyilawila said that is due to poor preparation by boxers themselves and their promoters because of not being serious in it.

“We have no enough preparation actually; you do exercises while thinking about other business. There is no way you can be perfect,” he added.

Saturday, 24 January 2015

OLIVEIRA: LUCAS SILVA NI 'ALMASI' KWA ANCELOTTI

Na Ramadhani Ngoda.
Real Madrid ikijiandaa kumtambulisha rasmi kiungo Lucas Silva siku ya Jumatatu baada ya kukamilisha usajili wake kutoka Cruzeiro ya Brazil, Kocha wake wa zamani Marcelo Oliveiro ameibuka na kusema kijana huyo ni kama almasi katika kikosi cha Carlo Ancelotti.
Lucas Silva

Lucas Silva Borges (21), ameigharimu Real Madrid kiasi cha yuro milioni 14 na kusaini mkataba utakaomuweka Bernabeu mpaka 2020.
 Oliveira ambaye ni kocha wa zamani wa kinda huyo amekitaja kitendo hicho kuwa ni utimilifu wa ndoto ya kijana huyo.
"Nimekuwa nikiongea na Silva, amekuwa mwenye furaha sana kwa moja ya ndoto zake kuwa kweli," alisema Oliveira.
Na sasa kijana huyo anaungana na Martin Odegaard ambaye naye ni ingizo jipya katika kikosi hicho cha mabingwa watetezi wa ligi ya mabingwa barani Ulaya.

ARSENAL NJIA NYEUPEEE KWA PAULISTA


Na Ramadhani Ngoda.
Bosi wa Arsenal, Arsene Wenger yuko katika harakati za kunasa saini ya beki wa kati kwa ajili ya kuimarisha safu yake ya ulinzi mwezi huu.
Na jicho lake limelenga kwa mlinzi wa kibrazil, Gabriel Paulista kutoka Vilareal ya Hispania.
Gabriel Paulista

  Ni kama mpango wa Arsenal kumsajili Paulista mwezi huu wa januari umepata nguvu baada ya beki huyo mwenye thamani ya paundi milioni 15 kuachwa katika kikosi cha Villarrealkinachoivaa Levante wikiendi hii.
 Villarreal walitangaza kikosi cha wachezaji 18 kinachochuana na Levante uwanja wa El Madrigal na waliorodhesha wachezaji watakaokosa mechi kwasababu ya majeruhi na kutumikia adhabu.

Japokuwa kuachwa kwa jina la Paulista, klabu haijatoa sababu katika tangazo lake, lakini  inaripotiwa kuwa nyota huyo yuko njiani kutimka. Na Emirates kunaweza kuwa fikizio lake.
Lakini  Arsenal wanaweza kukumbana na kikwazo kingine  kutoka kwa shirikisho la soka nchini Uingereza (FA) cha kupata kibali cha kazi kwa beki huyo raia wa Kibrazil.
Arsene Wenger- kocha wa Arsenal

Na Arsene Wenger amelilalamikia suala la utaratibu na kanuni za utoaji vibali kwa wachezaji wageni nchini Uingereza.

Thursday, 22 January 2015

PLUIJM UMEJIANDAA NA MECHI YA SIMBA?



Na Ramadhani Ngoda
Waswahili husema, “mazoea hujenga tabia”. Na hii ndio inayoonekana katika soka letu kwa sasa ambapo ambapo mambo madogo madogo hukomaa na kuwa tabia za vilabu vyetu hapa nchini jambo ambalo linapeleka soka la nchi hii kusiko.
Ni wazi sasa kauli ya kiingereza inayosema “they are hired to be fired” inayotafsirika “wanaajiriwa ili watimuliwe” inaonekana kuthibitika zaidi ktika soka.
Kutimuliwa kwa kocha wa Yanga Marcio Maximo ambaye pia aliwahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya Tanzania baada ya mchezo dhidi ya watani wao wa jadi Simba, ni sehemu ya utimilifu wa kauli hii.
Ni imani yangu kuwa uongozi wa klabu ya Yanga uliangalia uwezo wa kocha huyu hususani kipindi chake alichoinoa Taifa Stars na kujiridhisha kuwa anaweza kuwa mbadala sahihi wa kocha Ernie Brandts ambaye naye alikumbwa na “mafuriko” haya.
Nakumbuka jinsi ambavyo watu walivyofurika katika mitaa ya Twiga na Jangwani wakati wa kumpokea kocha Ernie Brandts, wengine wakianzia uwanja wa ndege wa J.K Nyerere kuonesha shauku yao kwa kocha huyu lakini ilimuwia kusahau mapokezi yote aliyopewa wakati anawasili baada tu ya mabao matatu ya Simba katika mchezo wa nani mtani jembe msimu uliopita. Brandts alifungashiwa akaenda.
Leo tunashuhudia Mbrazil Maximo aliyetua kwa mbwembwe katika kazi yake ya pili ya ualimu Tanzania akiongozana na Wabrazil wenzake Jaja na Coutinho naye anafungashiwa virago ugonjwa ukiwa ni ule ule ulioua kibarua cha Brandts wa mechi dhidi ya Simba.
Kocha wa Yanga, Hans Van Pluijm

Sasa pengo lake limezibwa na kocha aliyewahi kuinoa timu hiyo kabla ya kwenda Uarabuni kuinoa klabu ya Al Shoula, Hans Van Der Plujim.
Misemo ya wahenga bado itatawala ikiwemo huu “mwenzako akinyolewa zako tia maji”. Maneno haya ni vizuri aambiwe kocha Hans kutokana na yeye kurudi kuvaa viatu alivyoaviacha msimu uliopita na hajui kama vitakuwa saizi yake au vitakuwa aidha vikubwa ama vidogo kwake.
Na kama ugonjwa huu wa makocha kupoteza vibarua katika mchezo wa watani wa jadi, bado kuna mchezo wa Simba na Yanga wa ligi kuu katika mzunguko wa pili, je hautakuwa ‘ebola’ kwa kibarua chake?
Sote tunamtakia kila la kheri katika kibarua chake licha kutolewa katika robo fainali ya michuano ya mapinduzi lakini ana kila sababu ya kuliangalia hili.
Inaonekana kutolewa robo fainali mapinduzi si shida, wala sare na Ruvu si tatizo ila mchawi wa ni mechi ya Simba.
Na vilabu vyetu viweke wazi kuwa vinaajiri makocha kwa ajili ya michezo gani kwa sababu, tumeona Maximo ameiongoza Yanga kwenye michezo tisa akishinda mitano(ya mashindano) na kupoteza mitatu ukiwemo wa nani mtani jembe lakini pointi 15 alizovuna Mbrazili huyu zilionekana nyepesi kwenye mzani wa tathmini kuliko 9 alizopoteza ikiwemo pointi 3 za mchezo usio wa kimashindano(nani mtani jembe).
Sasa tujiulize, hata Maximo angeipa ubingwa Yanga na kupoteza mchezo dhidi ya Simba tu, pia angefungashiwa virago?
Ni kweli David Moyes alitimuliwa kutokana na kupoteza mchezo dhidi ya Manchester City? Mbona Mourinho hakutimuliwa wakati anatandikwa goli tano pale Camp Nou akiwa na Real Mdrid? Au mbona hatukuona kutimuliwa kwa Diego Simeone baada ya kupoteza kwa mabao 4-1 katika mchezo wa fainali wa ligi ya mabingwa dhidi ya wapinzani wao wa jadi Real Madrid kule Estadio  Da Luiz msimu uliopita?
Au kuna vipengele vya kimkataba wanavyosaini makocha hawa juu ya mchezo wa Simba na Yanga? Kunaweza kukawa na maswali mengi juu ya hili lakini bado kuna sababu ya jitihada za makusudi za kulinusuru soka la nchi yetu kwa kutafuta tiba ya’ugonjwa huu.