Na Ramadhani Ngoda.
Mshambuliaji wa Manchester United, Radamel Falcao, amepinga maneno yanayosemwa juu yake kuwa bado anasumbuliwa na majeraha kitu kinachosababisha ashindwe kufanya vizuri katika kikosi hicho kinachonolewa na Mdachi Louis Van Gaal.
Mshambuliaji wa Manchester United, Radamel Falcao, amepinga maneno yanayosemwa juu yake kuwa bado anasumbuliwa na majeraha kitu kinachosababisha ashindwe kufanya vizuri katika kikosi hicho kinachonolewa na Mdachi Louis Van Gaal.
![]() |
Radamel Falcao |
Falcao ambaye amepachika wavuni mabao matatu tu tangu awasili klabuni hapo kwamkopo akitokea AS Monaco ya Ufaransa bao la kwanza likiwa ni la mchezo dhidi ya Everton ambao Utd ilishinda kwa mabao 2-1, bado hajawa na kiwango kizuri kitu kinachosababisha mashabiki wengi wa Utd kuona kuwa wamelamba galasa kwa Mcolombia huyo.
Licha ya maneno mengi juu yake, Falcao amekuja juu na kusema kuwa wakati utafika na watu wataanza kushuhudia makali yake kutokana na juhudi na kujituma kwake uwanjani.
"Zilikuwa ni dakika 90 muhimu sana kwangu. Nahitaji kucheza na nafurahi kuwa nimecheza, Kwakweli, ni matumaini yangu ntaanza kufunga karibuni, lakini wakati utafika. Nina hakika na hilo," alisema Falcao baada ya mchezo dhidi ya QPR mwishoni mwa wiki.
Licha ya mshambuliaji huyo kujinasibu kuwa yuko fiti, kocha wake Louis Van Gaal amesema kuwa bado mchezaji huyo anatakiwa kuthibitisha uwezo wake zaidi ndani ya kikosi hicho ikiwemo kupachika mabao mengi kadri awezavyo .
Manchester Utd bado wanakabiliwa na sintofaham juu ya eidha kumpa mkataba wa kudumu mchezaji huyo aliyepata kung'ara na timu kamaAtletico Madrid na Monaco kabla ya kuumia goti lake na kukosa michuano ya kombe la dunia iliyofanyika mwaka 2014 nchini Brazil ama la.
No comments:
Post a Comment