Mino Riola ambaye ni wakala wa kiungo wa Juventus na timu ya taifa ya Ufaransa, Paul Pogba, amesema mchezaji huyo atakuwa sokoni majiraya joto na yoyote mwenye kitita cha kutosha anaweza kupata saini ya nyota huyo.
![]() |
Paul Pogba Kiungo huyo ambaye alijiunga na Juventus akitokea Manchester United mwaka 2012, amegeuka kuwa lulu nakuwindwa na vilabu mbalimbali vikubwa barani Ulaya ikiwemo klabu yake ya zamani Manchester United. Pamoja na baadhi ya vilabu kuhitaji huduma ya kiungo huyo mwezi Januari, Riola amezima ndoto hizo kwa kusema kuwa mteja wake ataondoka majira ya joto. Licha ya kusafisha njia kwa timu zinazomuwania Pogba, Riola ametandaza 'vipande vya chupa' kwa kusema kuwa timu inayomhitaji ni lazima iweke kitita cha kutosha. "Nataka klabu itakayomnunua imuamini na iwe tayari kulipa kwa ajili yake. Kwa anayemuhitaji inaweza kumuwia hata zaidi ya yuro milioni 100," alisema Riola. Ikumbukwe kuwa Pogba(21) ana mkataba na vibibi vizee hivyovya Turin mpaka 2019 na wakala wake huyo amsesema kuwa nyota huyo ana thamani na hadhi sawa na nyota wengine wakubwa duniani kama vile Messi, Cristiano Ronaldo, Zlatan Ibrahimovic na wengine. ![]() Kauli hiyo itawafanya Louis Van Gaal, Jose Mourinho, Laurent Blanc, Manuel Pelegrini na wengine kuvunja benki mwishoni mwa msimu kushinda vita ya kupata saini ya nyota huyo. |
No comments:
Post a Comment