Na Ramadhani Ngoda.
Bosi wa Arsenal, Arsene Wenger yuko katika harakati za kunasa saini ya beki wa kati kwa ajili ya kuimarisha safu yake ya ulinzi mwezi huu.
Na jicho lake limelenga kwa mlinzi wa kibrazil, Gabriel Paulista kutoka Vilareal ya Hispania.
![]() |
Gabriel Paulista |
Ni kama mpango wa Arsenal
kumsajili Paulista mwezi huu wa januari umepata nguvu baada ya beki
huyo mwenye thamani ya paundi milioni 15 kuachwa katika kikosi cha Villarrealkinachoivaa Levante wikiendi hii.
Villarreal walitangaza kikosi cha
wachezaji 18 kinachochuana na Levante uwanja wa El Madrigal na waliorodhesha
wachezaji watakaokosa mechi kwasababu ya majeruhi na kutumikia adhabu.
Japokuwa kuachwa kwa jina
la Paulista, klabu haijatoa sababu katika tangazo lake, lakini
inaripotiwa kuwa nyota huyo yuko njiani kutimka. Na Emirates kunaweza kuwa fikizio lake.
Lakini Arsenal wanaweza kukumbana na kikwazo kingine
kutoka kwa shirikisho la soka nchini Uingereza (FA) cha kupata kibali cha kazi
kwa beki huyo raia wa Kibrazil.
Na Arsene Wenger amelilalamikia suala la utaratibu na kanuni za utoaji vibali kwa wachezaji wageni nchini Uingereza.
Akisema kuwa zinatakiwa kufanyiwa marekebisho ili kuboresha ligi.
No comments:
Post a Comment