Saturday, 24 January 2015

OLIVEIRA: LUCAS SILVA NI 'ALMASI' KWA ANCELOTTI

Na Ramadhani Ngoda.
Real Madrid ikijiandaa kumtambulisha rasmi kiungo Lucas Silva siku ya Jumatatu baada ya kukamilisha usajili wake kutoka Cruzeiro ya Brazil, Kocha wake wa zamani Marcelo Oliveiro ameibuka na kusema kijana huyo ni kama almasi katika kikosi cha Carlo Ancelotti.
Lucas Silva

Lucas Silva Borges (21), ameigharimu Real Madrid kiasi cha yuro milioni 14 na kusaini mkataba utakaomuweka Bernabeu mpaka 2020.
 Oliveira ambaye ni kocha wa zamani wa kinda huyo amekitaja kitendo hicho kuwa ni utimilifu wa ndoto ya kijana huyo.
"Nimekuwa nikiongea na Silva, amekuwa mwenye furaha sana kwa moja ya ndoto zake kuwa kweli," alisema Oliveira.
Na sasa kijana huyo anaungana na Martin Odegaard ambaye naye ni ingizo jipya katika kikosi hicho cha mabingwa watetezi wa ligi ya mabingwa barani Ulaya.

No comments:

Post a Comment